Kutoka ‘SAYUNI POULTRY GOSHENI’ pekee tunakuletea
UTUNZAJI wa VIFARANGA ulio mwepesi kabisa tena wa gharama nafuu kabisa.
Hii sio ELIMU,
bali ni ubunifu tu utakaokuwezesha kuvuka na kupiga hatua. Utunzaji vifaranga
nao umekuwa changamoto kwa wafugaji wachanga ambao wengi wametawaliwa na hofu
ya kupata hasara. Hebu tujifunze pamoja.
Pichani hapo
chini ni picha ya banda (simple & local designed) lenye urefu wa inchi 50 na upana wa inchi 27 na kimo ni inchi 12. Limefunikwa chick-wire-mash upande wa juu na
pembezoni, ila kwa chini liko wazi, chini ni ARDHI, ni mchanga / udongo.
UKIPATA FUNDI MWAMINIFU AU UKIJISHUGHULISHA BINAFSI, GHARAMA YAKE HAIZIDI
15,000= au 20,000= ambayo ni faida sana ukilinganisha na gharama ya dawa, na ni
faida zaidi ikiwa utatunza vifaranga mara kwa mara.
Katika wiki
mbili za mwanzo vifaranga hushambuliwa sana na magonjwa ya mafua na/au miharo
ambayo yote husababishwa na uchafu kwenye mabanda. Na pia wiki mbili za mwanzo,
vifaranga huhitaji joto la kutosha kwa masaa yote 24 ya siku.
Ninapotumia
utunzaji huu; kwanza kabisa vifaranga vinapata HEWA halisi (free fresh air) moja kwa moja, tena
vinafurahia MWANGA na JOTO la JUA moja kwa moja, halafu vinafurahia ile ARDHI,
kwani kwao ni mpya/fresh kila siku (haina muendelezo wa kinyesi cha juzi wala
jana) na tena vifaranga hupendelea KUOGA kwenye mchanga (sand-bathing). Vifaranga
huwa salama dhidi ya kunguru nap aka na muda wote huonekana machoni
pako/mtunzaji (visible observed).
Wakati JUA
limekuwa kali sana, watengenezee KIVULI, (nusu KIVULI, nusu JUA, ili kuweza
kupata joto la wastani na mwanga wa wastani) ila hakikisha HEWA ya kutosha
inaingia. Usiogope ‘hasara’ ni sehemu ya kujifunza kutokana na makossa, ambayo next time/mara nyingine utakuwa
umeelimika.
Kwa utunzaji huu
‘simple & natural’, hakuna namna
itakayopelekea kutumia dawa za mafua au miharo na pia gharama za nishati (joto
na mwanga) zitashuka. Wakati wa usiku, italazimu kuvirudisha vifaranga vyako
kwenye banda la ndani au kwenye box. Zingatia USAFI, DAWA za KUANZIA na ratiba
ya CHANJO muhimu.
Jipatie “VIFARANGA 30” kwa bei ya OFA, na uweze
KUTUNZA VIFARANGA vyako kwa UHAKIKA
kabisa.
Kumbuka “VIFARANGA 30” ni UHAKIKA kulinganisha na KUTOTOLESHA MAYAI 30 kwani haukupi UHAKIKA
wa idadi ya vifaranga.
Ukipata “VIFARANGA 30” kwa UHAKIKA na elimu ya UTUNZAJI vifaranga kwa UHAKIKA hukupa MATOKEO ya UHAKIKA
katika UFUGAJI.
Ni wapi hapo? ni ‘SAYUNI POULTRY GOSHENI’ pekee inayokupatia
# VIFARANGA na tena # ELIMU ya UTUNZAJI VIFARANGA bure, na
tena # UTOTOLESHAJI wa MAYAI yako, na tena # ELIMU ya UTOTOLESHAJI bure, na tena # OFA za UTOTOLESHAJI, na tena #
USHAURI wa MIFUGO bure, na tena # HUDUMA
kwa WATEJA bure kwa njia ya simu, na tena # Mambo mengine meeeengi… .
…usisite
kumjulisha na jirani/rafiki/jamaa zako. Soma
makala kamili ya UTUNZAJI VIFARANGA.
No comments:
Post a Comment